*Pata habari zote za hapa mjini Dodoma (Capital City) na nyinginezo kutoka MIJI mbalimbali hapa Tanzania na nje ya Tanzania* >>>>>>> *Pata habari zote za hapa mjini Dodoma (Capital City) na nyinginezo kutoka MIJI mbalimbali hapa Tanzania na nje ya Tanzania*

  • Thursday, 2 April 2015

    Maamuzi ya tume ya uchaguzi kuhusu kura ya maoni ya katiba iliyopendekezwa…

    lunMoja ya ishu ambazo zimeleta mvutano mkubwa bungeni ni mjadala kuhusu usajili wa wapiga kura kwa mfumo wa kielektroniki BVR na ishu ya kupigia kura katiba iliyopendekezwa.
    Jana kulitokea mvutano Bungeni baada ya Mbunge John Mnyika kuomba mwongozo kuhusu changamoto zilizojitokeza kwenye mfumo wa usajili wa BVR.
    Taarifa iliyotufikia ni kwamba Mwenyekiti wa ya tume ya uchaguzi Tanzania, NEC Jaji Damian Lubuva ametangaza kuahirishwa kwa mchakato wa kupiga kura ya maoni ya katiba iliyopendekezwa hadi hapo tarehe mpya itakapotangazwa tena.
    Wadau mbalimbali wa siasa wamekua wakitoa maoni yao kuhusu kura ya maoni iliyopangwa kufanyika April 30 huku wengi wakidai ni vigumu zoezi hilo kufanyika kwa wakati kutokana na sababu mbalimbali.

    0 comments:

    Post a Comment