Ilianza kama ishu ya kawaida hivi lakini
muda ulivyozidi kwenda ikazidi kuchukua headlines kwenye mitandao ya
kijamii kwamba eti kuna watu wananunua sarafu za shilingi mia tano za
Tanzania alafu wanatumia madini ya sarafu hiyo kutengeneza vito kama
mikufu hivi !
Nimepitia kwenye channel ya Youtube ya blogger mkubwa Tanzania, Issa Michuzi >>>Michuzi TV na nimekutana na hii stori nikaona niisogeze hapa kushare na wewe pia.
Anayehojiwa ni Abdul M. Dollah ambaye ni Meneja Msaidizi wa Huduma za Kibenki Benki Kuu TZ… Majibu yake ni haya kuhusu hiyo ishu; “Huu
uvumi tumeusikia wananchi wengi wanakuja na kuulizia habari hiyo, huo
ni uvumi tu na sio kweli kwamba kuna madini yoyote katika hii sarafu ya
mia tano ambayo yanaweza kutengeneza vito vya thamani” >>> Abdul M. Dollah
“Wakati
tunaizindua hii sarafu mwaka jana tuliwaambia kwamba humu ndani kuna
madini yya chuma kwa asilimia 94 na madini ya Nikel asilimia sita
tu… Benki Kuu inaamini kwamba Wananchi wanadanganywa” >>> Abdul M. Dollah
0 comments:
Post a Comment