Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania - NEC, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Damian Lubuva. |
Zoezi
hilo lilizinduliwa Februari 24 mwaka huu katika halmashauri ya mji wa
Makambako na kisha kuendelea katika halmashauri zote za mkoa wa Njombe.
Uandikishwaji huo unatarajia kumalizika April 15 na kwamba kata
zilizo salia kila halmashauri zimeanza kukamilisha uandikishaji ambapo
katiaka halmashauri ya mji wa Njombe, kata za Ramadhani na Njombe mjini
zilizowekwa kipolo zimeanza uandikishaji.
EATV imepita katika vituo mbalimbali ndani ya kata za Njombe Mjini na
Ramadhani hususani vituo vilivyopo mitaa ya Kibena na Idundilanga na
kujionea foleni ndefu ambayo bado imeendelea kuzua malalamiko kwa baadhi
ya wakazi ambao wanaiomba tume kubadili ratiba ya kufungua vituo kwani
wamekuwa wakifika usiku kujiandikisha huku vituo vikifunguliwa saa mbili
kama ilivyopangwa.
Lameck Ulaya ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Idundilanga ambao una jumla ya
vituo vinne ya kuandikisha ambapo amesema huenda wananchi wakawa na
dhamira ya dhati katika kuwapata viongozi wao Kktika uchaguzi mkuu wa
Oktoba, kutokana na mwamko mkubwa wa jamii kujitokeza katika vituo vyao
pamoja na kuhimiza wananchi wengi kuendelea kujitokeza
Katika kata za Njombe Mjini zoezi hilo linaonekana kuwa na mafanikio
makubwa kutokana na tume kuamua kuwatumia waandikishaji kutoka kata
nyingine ambao wana uzoefu na mashine za BVR ambapo zaidi ya watu 150
wanaandikishwa katika vituo kwa kila kituo kwa siku.
0 comments:
Post a Comment