*Pata habari zote za hapa mjini Dodoma (Capital City) na nyinginezo kutoka MIJI mbalimbali hapa Tanzania na nje ya Tanzania* >>>>>>> *Pata habari zote za hapa mjini Dodoma (Capital City) na nyinginezo kutoka MIJI mbalimbali hapa Tanzania na nje ya Tanzania*

  • Thursday, 9 April 2015

    Ajali nyingine leo TANGA, mabasi mawili na gari ndogo, kuna vifo na majeruhi..RIP

    IMG-20150409-WA0013
    Tangu ilipotokea ajali ya barabarani eneo la Changarawe Iringa ambayo ilitokana na basi la abiria la Kampuni ya Majinjah Express kugongana na lori, stori zikaendelea kuwa nyingi kwenye vyombo vya habari, nyingi zikiandikwa kuhusu vyanzo vya ajali hizo.
    Ajali nyingine tena imetokea Tanga leo APRIL 9 2015, taarifa za awali zinasema watu 10 wamefariki na wengine wamepata majeraha kutokana na ajali hiyo iliyotokea eneo la Mkata, Wilaya ya Handeni Tanga, gari zilizopata ajali hiyo ni basi la NGORIKA, jingine la RATCO pamoja na gari nyingine ndogo.
    Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, RPC Juma Ndaki kathibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akisema kwamba mwendo kasi umechangia kutokea ajali hiyo.

    Hizi ni PICHA ambazo zimeenea mitandaoni zikionesha jinsi hali ilivyo eneo la tukio.
    IMG-20150409-WA0014 
    IMG-20150409-WA0016
    IMG-20150409-WA0017
    IMG-20150409-WA0018
    IMG-20150409-WA0019#RIP kwa watu wetu waliofariki kwenye ajali hiyo, pole kwa waliopata majeraha pia.

    0 comments:

    Post a Comment