
Mmiliki wa kampuni ya
Microsoft
Bill Gates amekunywa maji yaliotengenezwa kutokana na kinyesi cha
binaadamu kama maonyesho ya teknolojia mpya itakayoweza kutoa maji safi
katika Mataifa yanayoendelea.Mwanzilishi huyo wa kampuni ya
Microsoft amesema kuwa ataisambaza mitambo ya teknolojia hiyo mpya kote
duniani baada ya kuifanyia majaribio na kuridhika nayo mwishoni mwa
mwaka huu.Teknolojia hiyo imeungwa mkono na shirika la
WaterAid ambalo limesema kuwa litasaidia sana katika maeneo ya mengi ya miji.Kulingana na shirika hilo takriban watu millioni
748 hawana maji safi ya kunywa.Katika kanda ya video iliyowekwa katika blogu yake,
Bill Gates
alishuhudia kinyesi cha Binaadamu kikiingizwa katika mtambo huo kabla ya
kunywa maji yaliokuwa yakitoka baada ya kuboreshwa ambapo huchukua
dakika tano kukamilika.
0 comments:
Post a Comment