*Pata habari zote za hapa mjini Dodoma (Capital City) na nyinginezo kutoka MIJI mbalimbali hapa Tanzania na nje ya Tanzania* >>>>>>> *Pata habari zote za hapa mjini Dodoma (Capital City) na nyinginezo kutoka MIJI mbalimbali hapa Tanzania na nje ya Tanzania*

  • Thursday, 8 January 2015

    Hii ni taarifa ya Mwanamke aliyekua Sister kupewa upadri…asema yupo tayari kutengwa na kanisa


    padri2Pamoja na kwamba sheria za kanisa katoliki haziruhusu mwanamke kuwa padri lakini mwanamke aliyetambuliwa kwa jina la Georgia Walker amepewa cheo cha upadri katika jimbo la Kansas nchini Marekani,tukio ambalo ni la kwanza kwa kanisa katoliki.Mwanamke huyo mwenye miaka 67 ambaye awali alikuwa mtawa wa kike maarufu sista alipewa daraja hilo jumamosi iliyopita lakini upadrisho wake uliingia kwenye mzozo baada ya uongozi wa kanisa lake kudai hautambui kuapishwa kwake.
    tayarKutokana na hatua hiyo sista huyo anaweza kutengwa na kanisa kutokana na ukweli kuwa sheria za kanisa zinasema mwanamke hawezi kuwa padri.Lakini kwa upande wake alipingana nao na kusema haoni sababu za kukataliwa kuwa padri kwani Yesu alifundisha watu wote bila kubagua jinsia wala hadhi zao.Ibada ya upadrisho iliongozwa na Askofu Bridget Mary Meehan wa Chama cha Mapadri wanawake wa kanisa Katoliki na wakati akipewa upadri hakuonyesha hofu yoyote na alionekana akisema hatishiwi na hatua ya kanisa kumtenga.

    0 comments:

    Post a Comment