Hizi ni baadhi ya picha za tukio zima lilivyofanyika la kumpokea Baba Askofu Mkuu wa Jimbo Jipya la DODOMA (Dodoma,Singida na Kondoa) Beatus Kinyaiya ,Tarehe 17-18/01/2015,ambalo mwanzo lilikua Chini ya Jimbo Kuu la DAR ES SALAAM.
Picha hii Kushoto akiwa amekaa Askofu Mkuu Beatusi Kinyaiya na kulia akiwa amekaa askofu wa jimbo la Mwanza Askofu Luaichi ambaye alishawahi kuwa askofu wa jimbo la Dodoma.
Mambo yalikuwa kama ifuatavyo:-
1. Tarehe 17/01/2015 ndio ilikua siku ya kumpokea baba askofu
2. Tarehe 18/01/2015 ndiyo ilikua siku ya kusimikwa jimbo na askofu mkuu BEATUSI KINYAIYA
![]() |
Baada ya kupokelea sasa anatoa neno la shukrani kwa watu wa DODOMA na Baraka |
![]() |
Spika wa Bunge Mh. Anna Makinda pia alikuwepo katika sherehe hizo siku ya Tarehe 17/01/2015 |
![]() |
Father Chesco na Mh Anna Makinda wakiwa wanasali kupokea baraka za Askofu Mkuu wa Jimbo la Dodoma. |
![]() |
Msafara wa Mapadri na Maaskofu kutoka Majimbo Tofauti tofauti ukielekea Sehemu iliyoandaliwa kwaajili ya Ibada ya kusimikwa Baba Askofu Beatusi Kinyaiya na Jimbo. |
![]() |
Mwakilishi wa Papa Akisoma hati ya Kusimikwa Jimbo la Dodoma kuwa Jimbo KUU |
![]() |
Raisi Mstafu Mh.Benjamini William Mkapa na Mke wake wakiwa katika IBADA takatifu ya kumsimika Askofu na Jimbo Kuu |
0 comments:
Post a Comment