*Pata habari zote za hapa mjini Dodoma (Capital City) na nyinginezo kutoka MIJI mbalimbali hapa Tanzania na nje ya Tanzania* >>>>>>> *Pata habari zote za hapa mjini Dodoma (Capital City) na nyinginezo kutoka MIJI mbalimbali hapa Tanzania na nje ya Tanzania*

  • Friday, 23 January 2015

    Mitandao ya Kijamii ni Kipimo cha STRESS na PRESSURE>>>>

    TwitterMoja ya Teknolojia inayokua kwa kasi ni matumizi ya mitandao ya kijamii duniani kote ambapo kwa sasa mamilioni ya watu wamekua wakitumia mitandao hiyo kuwasiliana.
    Lakini unaambiwa watafiti kutoka Australia wamegundua kuwa matumizi ya mitandao husaidia kumtambua mgonjwa wa moyo pamoja na mtu mwenye stress kwa asilimia kuwa.
    Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Melbourne na Pennsyvania, Marekani unaonyesha kuwa post za kwenye kurasa za mitandao kama Twitter sio tu zinaweza kuonyesha hatari ya ugonjwa wa moyo lakini pia zinaweza kutumika kama kipimo cha saikolojia.
    melMatokeo ya utafiti huo ambayo yatachapishwa wiki ijayo katika jarida la kisayansi  yameonyesha kuwa kutumia maneno mazuri katika mitandao kunaweza kubainisha mambo mengine yanayohusu afya ya mtu.
    Mfano kwenye ukurasa wa Facebook sehemu ya kuandika post, kuna option imeandikwa ‘Add what you’re doing or feeling, ukiandika annoyed’, ‘sad’ au ‘emotional moja kwa moja inahusisha na hatari ya kupata magonjwa ya moyo, lakini maneno ‘blessed’, ‘loved’ au ‘happy yanakuweka kwenye hatari ndogo ya magonjwa hayo.

    0 comments:

    Post a Comment