
Kikao cha Makamishna wa Jeshi la Polisi
kinachofanyika Dodoma leo kinafikia mwisho, tuliona jinsi ambavyo Benki
ya NMB ilikuwa nao bega kwa bega kuanzia siku ya kwanza Kikao hicho
kilipoanza siku ya Jumatatu January 26.
Mbali na ufadhili uliofanywa na Benki
hiyo kutoa mil. 75 kwa ajili ya kikao hicho, NMB ilikuwa ikitoa huduma
mbalimbali katika mabanda yaliyowekwa nje ya ukumbi wa St. Gaspar,
Dodoma.
Moja ya huduma ambazo zilitolewa katika mabanda hayo ni kutoa na kuweka fedha kupitia NMB wakala ambapo kupitia teknolojia ya Max Malipo,
mteja anaweza kutoa na kuweka fedha na pia kupata huduma zingine za
kibenki ambazo angeweza kuzipata katika tawi lolote la NMB hivyo
walijionea jinsi ambavyo huduma hiyo imerahisisha huduma za NMB karibu
nao.
![]() |
Meneja Mwandamizi katika kitengo cha wateja binafsi Suzan Shuma akimjazia fomu Kamishna wa Polisi kutoka makao makuu ya jeshi la Polisi, Paul Chagonja, fomu itamrahisishia kupata taarifa fupi za akaunti yake ya NMB kupitia mtandao wa E-mail (E-statement). |
![]() |
Kamishna wa Polisi Paul Chagonja, Kamanda Thobias Angengeye pamoja na Meneja Mwandamizi katika kitengo cha wateja binafsi, Suzan Shuma. kwenye banda la Huduma za NMB Dodoma. |
0 comments:
Post a Comment