*Pata habari zote za hapa mjini Dodoma (Capital City) na nyinginezo kutoka MIJI mbalimbali hapa Tanzania na nje ya Tanzania* >>>>>>> *Pata habari zote za hapa mjini Dodoma (Capital City) na nyinginezo kutoka MIJI mbalimbali hapa Tanzania na nje ya Tanzania*

  • www.DomPromo.blogspot.com

    This is a blog that shows the various issues of Dodoma to advertise various business undertaken in Tanzania with....

    This is a better FOOD found at MBALAMWEZI Restaurant

    Mbalamwezi Restaurant found at Dodoma-Mtendeni Street, Dodoma Work Time:- Open today · 6:30 am – 10:00 pm .

    Dodoma Dance Competition at MATEI LOUNGE

    Kiingilio ni Kinywaji chako tu....... MATEI LOUNGE Best place for Enjoying

    ROYAL VILLAGE HOTEL-DODOMA

    Welcome to one of Hotel found at Dodoma (Royal Village Hotel). It offers the friendliest of Tanzania hospitality. The hotel has a number of rooms; Suite and Deluxe. All are self-contained with AC and TV connected to DSTV.

    SINGSUNG Electronics Shop

    A big shop found at DODOMA that sales electronics divices,Found at Mtendeni Street near New MAISHA CLUB for more details call 0757575144.

    SHABIBY LINE

    We provide BUS services daily contact with us,We are the Best in Dododma.

    Tuesday, 8 November 2016

    Album ya Drake “Views” imekuwa tishio, rekodi nyingine imetengenezwa kwenye Spotify

    Kwa sasa ukitaka kuwataja wasanii wa HipHop ambao wamepata mafanikio makubwa katika Album zao basi jina la Drake haliwezi kukosekana. Image result for drake views spotify
    Baada ya mtandao wa Apple Music kuitangaza Album ya Drake “Views” kuwa ndio album ya kwanza kufikisha wasikilizaji Bilioni moja, nyimbo ya One Dance kusikilizwa mara Milioni 924 katika mtandao wa Spotify, kuvunja rekodi ya Michael Jackson kwa kutajwa katika vipengele vingi vya tuzo za AMA’S, Sasa Good newz nyingine ni kwamba mtandao wa Spotify umetangaza kwamba Album ya “Views” imekuwa stream mara Bilioni 3.
    Image result for drake views spotify
    Na jingine la kufahamu kutoka kwa Drake ni kwamba anajiandaa kuachia project yake ampya akiwa na Kanye West.

    Wednesday, 16 March 2016

    Simu zitakazotupwa na WhatsApp

    Wakati wa kuanzishwa kwa WhatsApp, simu nyingi za smartphone zilikuwa za Blackberry na Nokia
    Huduma ya WhatsApp haitatumika tena katika simu zinazotumia mifumo kadha ya programu ikiwemo Blackberry 10, Nokia Symbian S60 na Windows Phone 7.1.
    Kampuni ya Facebook inayomiliki huduma hiyo imesema inataka kuangazia kustawisha “huduma katika mifumo inayotumiwa na watu wengi.”
    WhatsApp, itaacha kufanya kazi katika mifumo hiyo ya programu kufikia Desemba 2016.
    Licha ya kuacha kutumika katika simu nyingi za Blackberry, WhatsApp bado itaendelea kutumiwa katika simu za kisasa zaidi za Blackberry kwa sababu simu hizo hutumia mfumo wa Android.
    Kampuni hiyo imejitetea na kusema kwamba haijawatupa wateja wake ambao wamechangia sana katika ufanisi wake lakini ni kutokana na mabadiliko ya teknolojia.
    “Simu hizi hazina uwezo wa kiteknolojia tunaohitaji kuendelea kuimarisha huduma yetu siku zijazo,” kampuni hiyo imesema.
    WhatsApp hutumiwa na watu bilioni moja duniani
    Orodha kamili ya mifumo ya simu ambayo wateja hawataweza tena kutumia WhatsApp ni hii hapa:
    • Android 2.1 and Android 2.2
    • Blackberry OS 7 and earlier
    • Blackberry 10
    • Nokia S40
    • Nokia Symbian S60
    • Windows Phone 7.1
    Kampuni hiyo imesema wakati wa kuanzishwa kwa WhatsApp mwaka 2009, asilimia 70 ya simu wakati huo zilikuwa za BlackBerry na Nokia."
      Simu ya Blackberry
    Lakini sasa asilimia 99.5 ya simu zinatumia mifumo ya Google, Apple na Microsoft.

    Friday, 8 January 2016

    Shehena ya Petroli Fake yazuiwa


    Posted by:HABARI LEO 

    SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS), limeamuru shehena ya mafuta ya petroli iliyoagizwa kutoka Falme za Kiarabu irejeshwe ilikotoka kutokana na kubaini hayana ubora unaotakiwa kwa matumizi ya magari na mitambo.


    Akitoa taarifa hiyo Dar es Salam jana, Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Joseph Masikitiko alisema, vipimo vya maabara vya sampuli ya mafuta hayo vimeonesha kuwa hayafai kwa matumizi. Alisema hayo ni matokeo ya ukaguzi wa hivi karibuni wa shehena hiyo yenye ujazo wa tani za metriki 38,521.018 katika meli ya MT. Ridgebury John B, yaliyokuwa yasambazwe na kuuzwa nchini.

    Alisema, "Vipimo vinaonesha kuwa baadhi ya matakwa ya viwango vya mafuta ya petroli hayajafikiwa, hivyo kuamuru yarejeshwe yalikotoka. Kiwango cha ubora cha mafuta ya petroli ni TZS 672:2012/ EAS 158:2012 ambacho hakikufikiwa".

    Matakwa ya kiwango ambacho mafuta hayo hayakukidhi ni pamoja na kuwa na kemikali zilizo na oksijeni ndani yake ambazo husababisha madhara kwenye injini za magari na mitambo.Alisema, "Kiwango cha petroli hakiruhusu uwepo wa kemikali hizo kwenye mafuta hayo kwa sababu zinaua injini, kuhatarisha afya za watu na kuharibu mazingira kutokana na kusababisha moshi mchafu mwingi".

    Alifafanua kuwa mafuta hayo yameonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kuvuta maji au mvuke na kuwa sehemu ya petroli, kiasi cha kuifanya iwe na maji mengi ambayo ni hatari kwa injini za magari na mitambo.

    Pia, alieleza uhafifu mwingine katika mafuta hayo kuwa ni kupungua kwa nguvu ya kuendesha injini au mitambo hivyo kusababisha uharibifu na hasara. Aliongeza kuwa, mvuke unapokuwa mwingi kwenye petroli husababisha mtiririko wa mafuta kwenda kwenye injini kutokuwa mzuri, huku kemikali aina ya benzene iliyoonekana kuzidi katika petroli hiyo ikiwa ni chanzo cha kansa kwa wanaotoa huduma ya uuzaji wa mafuta hayo.

    Sambamba na hayo, Masikitiko aliongeza kuwa walibaini kuwa uhafifu katika mafuta hayo unaongeza wingi wa ujazo wa nishati hiyo pasipokuwa na uhalisia na kisha kutoa nguvu isiyolingana na wingi wake. Alisema, madhara yake ni mnunuzi kulipia wingi wa mafuta usio na thamani halisi.Aliwahakikishia watumiaji wa mafuta kuwa, shirika hilo litahakikisha linafanya ukaguzi katika meli zote zenye mafuta yanayokusudiwa kusambazwa nchini ili kuzuia yasiyo na ubora yasiingizwe sokoni.

    Katika hatua nyingine, Tbs ilisema kuwa iliagiza vilainishi vya mitambo na magari vya kampuni ya HASS Petroleum (T) Limited vyenye ujazo wa lita 16,080 kutoka Falme za Kiarabu virejeshwe vilikotoka pia kwa sababu ya kukosa ubora unaofaa kwa matumizi na kwamba mwagizaji alitekeleza agizo hilo tangu Desemba 31 mwaka jana.

    Ewura yazungumza Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) imekiri kufahamu kuhusu suala hilo na kueleza wananchi kuwa licha ya mafuta hayo kutakiwa kurejeshwa yalipotoka, bado nchi ina akiba ya petroli inayoweza kutumika hadi shehena nyingine iletwe."Wananchi wasiwe na wasiwasi," alisema Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa Ewura, Titus Kaguo. Alisema kwa siku nchi inatumia lita za petroli 2,700,000, na kwamba kila metriki tani moja ya petroli huwa na lita 700,000.

    "Kwa maana hiyo, lita 33,000,000 za petroli zilizokuja na kukataliwa endapo zingeshushwa na kutumika nchini zingeweza kutosheleza mahitaji kwa zaidi ya siku saba," alisema Kaguo . Hata hivyo, aliongeza kuwa si mafuta yote yanayoingia na meli bandarini hushushwa kwa ajili ya matumizi ya nchi, bali mengine huwa safarini kwenda nchi nyingine.

    Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu dompromo92@gmail.com au Whatsapp namba +255759399445.

    Thursday, 8 October 2015

    Shuhudia Laptop ya kwanza ya Microsoft kwenye muundo wa pekee kabisa… (Pichaz & Video)

    Kwa sababu kila mtu anahitaji kuwa na kifaa kizuri cha Mawasiliano, nimeona kuna umuhimu pia uipate na hii mpyampya kutoka Kampuni ya Kampuni ya Microsoft, Marekani.
    Microsoft ni kampuni ambayo imewekeza sana kwenye Teknolojia, walianza na biashara ya kutengeneza program za Computer, baadae wakaendelea kukuza biashara yao… mwaka 2014 Microsoft waliamua kuinunua pia Kampuni ya Nokia na kuendelea na Biashara ya uzalishaji wa Simu.

    New York City - October 6, 2015 The Microsoft Surface Book is displayed at the Microsoft Windows 10 Devices Media event in New York City. Credit: Andrew White for WIRED
    Kipya kinachokuja ni hii laptop mpya, imepewa jina la Microsoft Surface Book, hii ni zaidi ya laptop ya kawaida, ina uwezo wa kutumika kama Laptop au unaitenganisha alafu inakuwa Ipad… hii itakuwa ya kwanza kabisa kutengenezwa na Kampuni hiyo ya Microsoft.
    New York City - October 6, 2015 Panos Panay introduces the Microsoft Surface Book at the Microsoft Windows 10 Devices Media event in New York City. Credit: Andrew White for WIRED
    Unaambiwa kama ikijaa chaji ina uwezo wa kufanya kazi mpaka kwa saa 12, mpango walionao ni kuitambulisha na kuiingiza rasmi sokoni kuanzia October 26 2015 na itauzwa kwa Dola 1,499 ambazo zinagusa kama Milioni 3.2.
    New York City - October 6, 2015 The Microsoft Surface Book is displayed at the Microsoft Windows 10 Devices Media event in New York City. Credit: Andrew White for WIRED
    Ukiangalia hata sehemu inapojikunjia imekaa tofauti na nyingine nyingi tulizowahi kuziona mtu wangu.
    New York City - October 6, 2015 The Microsoft Surface Book is displayed at the Microsoft Windows 10 Devices Media event in New York City. Credit: Andrew White for WIRED
    New York City - October 6, 2015 The Microsoft Surface Book is displayed at the Microsoft Windows 10 Devices Media event in New York City. Credit: Andrew White for WIRED
    Iko na video yake pia hapa kwenye sekunde 96.......
    https://youtu.be/XVfOe5mFbAE

    Tuesday, 4 August 2015

    BARAZA KUU LA CHADEMA LARIDHIA DKT SLAA KUPUMZIKA.

    Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu dompromo@gmail.com au Whatsapp namba +255759399445. 


    Hatimaye baraza kuu la Chadema limeridhia kusimama kwa muda kufanya kazi za chama aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho Dr Wilbrod Slaa.
    Ni kishindo cha baraka za baraza kuu la Chadema likiridhia kupumzika kwa Dk Wilibroad Slaa ambaye tangu kujiunga kwa wazir mkuu mstaafu Edward Lowassa amekuwa haonekani katika vikao vyetu vya chama hicho, katika ufunguzi wa mkutano wa baraza kuu la Chadema mwenyekiti wa chama hicho taifa Freeman Mbowe amekiri kuwa licha ya Dkt Slaa kushiriki vikao mbalimbali vya chama kuhusu ujio wa lowassa, lakini ni kweli alitofautian kimtizamo na wajumbe wa kamati kuu. 
    Aidha Freeman Mbowe amekiri pia juu ya hofu iliyokwisha kutanda kwa viongozi, wanachama na wapenzi wa chama hicho juu ya ujio wa baadhi ya vigogo kutoka ndani ya chama cha mapinduzi CCM.
    Kwa upande wake kaimu katibu mkuu wa Chadema taifa Salum Mwalimu akizungumza katika mkutano huo pamoja na masuala mengine amewataka wanachama na wapenzi wa chama hicho kuahkikisha wanaunganisha nguvu hasa katika kipindi cha uchaguzi.
    Miongoni mwa agenda kuu zilizojadiliwa katika baraza kuu la Chadema ni pamoja na agenda ya kupitisha ilani ya chama hicho, kupendekeza majina ya wagombea nafasi ya urais ikiwa ni pamoja na kuthibitisha mikakati na rasilimali za kuendesha kampeni za uchaguzi mkuu.

    Thursday, 30 July 2015

    Maelezo yaliyotolewa na Polisi Dodoma kuhusu Naibu spika Job Ndugai kumpiga mtu mpaka akazimia.

    Ndugai 1Stori ilianza kusambaa kuanzia July 28 2015 kwamba Naibu spika wa bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania Job Ndugai amempiga mtu mpaka akazimia na kisha baadae kufariki.
    Hili tukio limefanya mpaka millardayo.com imtafute kamanda wa Polisi Dodoma Kamishna msaidizi mwandamiz wa Polisi David Misime ambaye ameyathibitisha haya >>> ‘Ukweli nilionao mimi ni kwamba tarehe 28 2015 jioni Joseph Elieza Chilongale alifika kwenye kituo cha Polisi Kongwa Dodoma akilalamika kuwa wakiwa kwenye mkutano wa kujinadi kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea Ubunge jimbo la Kongwa kupitia CCM, alipigwa kwa kutumia fimbo kichwani na tumboni na Job Ndugai
    Baada ya kutoa taarifa hiyo alipewa PF3 na akapelekwa Hospitali ambako amelazwa, tunachofanya ni kuendelea na uchunguzi kwa kupata maelezo kutoka kwenye eneo la tukio kutoka kwa watu waliokuwepo pale na baada ya kukamilisha upelelezi tutafikisha jalada kwa Mwanasheria wa serikali aelekeze hatua za kuchukua‘ – Kamanda Misime.
    Kuhusu taarifa kwamba Joseph amefariki, Kamanda Misime amesemahizo taarifa sio za kweli sababu mkuu wa Upelelezi wilaya ya Kongwa muda mfupi uliopita alikua pale Hospitali kuchukua maelezo yake kwa ajili ya kukamilisha upelelezi

    Bweni la shule ya Wiliam Lukuvi laungua tena


    Bweni la moja la Shule ya Sekondari Wiliam Lukuvi iliyopo taarafa ya Pawaga wilayani Iringa vijijini, limeteketea kwa moto na kusababisha uharibifu wa vitu mbalimbali ikiwemo vitanda.Kaimu Kamanda Pundensiana Protas amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema hakuna mtu ambaye ameathirika kutokana na ajali hiyo.
    Kaimu Kamanda Pundensiana Protas amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambaopo amesema hakuna mtua ambaye ameathirika kutokana na ajali hiyo.

    Wednesday, 1 July 2015

    MAGAZETINI JULY1..Maiti yatoa jasho na kutikisika, Bei ya Petrol haishikiki na kidato cha 5 wakosa nafasi.

    HIGH 
    MTANZANIA
    Hali ya sintofahamu imeibuka katika eneo la Magomeni, Wilaya ya Bagamoyo baada ya mwili wa marehemu Hatujuani Shaaban kushindikana kuzikwa kutokana na ndugu zake kudai ulikuwa ukitokwa jasho, kutingisha miguu, kichwa na mikono wakati ukitayarishwa kwa maziko.
    Kutokana na hali hiyo mwili huo ambao ulikuwa uzikwe jumapili uliachwa hadi jana baada ya daktari kuitwa na kuishauri familia, ndipo zoezi la mazishi likafanyika.
    Hatujuani alifariki dunia katika hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo jumapili saa mbili asubuhi na mwili wake kukabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya taratibu za mazishi.
    Ndugu yake aitwaye Mlau Mzee alisema walipofika nyumbani maandalizi ya mazishi yalianza kufanyika kwa taratibu za dini ya kiislamu na walitarajia kuuzika siku hiyo hiyo ya jumapili.
    Alisema taratibu za kuosha mwili wa marehemu zilishindikana  kutokana na maiti hiyo kujinyoosha, kutikisa kichwa na mguu wa kulia hali iliyowafanya wasitishe zoezi hilo na kumwita daktari.
    Mzee alisema baada ya mwili huo kaachwaa juzi, hatimaye jana waliamua kumsafisha tena ambapo marehemu alitikisa tena mkono na ndugu kuamua kuwaita waganga wa kienyeji.
    Daktari msadizi wa hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo Ally Ponza alikiri kutokea kwa kifo cha mtu huyo baada ya kumpokea akiwa na malaria kali na baadaye alifariki.
    Alisema alipigiwa simu na muuguzi kuwa mama huyo amefariki na yeye kwenda kumpima na kuhakikisha amefariki kabla ya kuwaambia ndugu zake.

    MTANZANIA
    Mbunge wa Igunga Peter Kafumu na Naibu Waziri wa Nishati na madini  Charles Mwijage nusura wazichape jana bungeni baada ya kurushiana maneno makali bungeni.
    Tukio hilo lilitokea wakati wa semina ya kujengewa uelewa kuhusu miswada mitatu iliyotarajiwa kuwasilishwa kuanzia leo hadi Julai 6 kwa hati ya dharura.
    Miswada hiyo ni sheria ya Petrol, usimamizi wa mapato ya mafuta na muswada wa sharia ya uwazi na uwajibikaji katika tasnia ya uchumbaji Tanzania ya mwaka 2015.
    Dk.Kafumu akichangia alisema sheria hizo zinahitaji muda ili zitazamwe vizuri na kwamba zikiharakishwa zitasababisha matatizo makubwa.
    Kauli hiyo ilisababisha Mwijage kutaka kumpiga Mbunge huyo baada ya kuwapo kwa majibizano makali kati yao.
    Mwijage alinyanyuka na kumnyooshea kidole Kafumu kwa ukali huku akizungumza maneno ambayo hayakusikika na tafrani hiyo iliendelea kwa muda huku baadhi ya Wabunge wakimzoe Naibu Waziri huyo.
    Mwenyekiti wa kamati ya Bunge Richard Ndassa alimwamuru Mwijage akae chini na ajiheshimu kwa kuwa ndani ya ukumbi huo kulikuwepo na bosi wake ambaye ni Waziri Nishati na Madini George Simbachawene.
    “Mhe. Waziri ongea na kiti na sio Mbunge, na usimnyooshee mwenzako kidole, na ukumbuke wewe ni Naibu Waziri na Waziri wako yuko hapa”Ndassa.
    JAMBOLEO
    Wabunge wanatarajia kupata mafao yao kuanzia Jula 10 baada ya Jakaya Kikwete kuvunja Bunge Julai 9 mwaka huu, Dodoma.
    Wabunge wametoa mapendekezo ya kutaka kuongezewa mafao yao ya hitimisho la Bunge la 10, ambapo sasa kila Mbunge atalipwa kiasi cha zaidi ya milioni 238 na kwa idadi ya Wabunge wote Hazina itapaswa kuwalipa wabunge jumla ya shilingi 85,024,548,,000.
    Kaimu katibu wa Bunge Kitolina Kippa alisema mafao ya Wabunge yatatolewa baada ya Bunge kuvunjwa iwapo Hazina itakuwa imekamilisha utaratibu mzima wa malipo hayo.
    Alisema kwa sasa bunge linaendelea na vikao vyake na kukana taarifa za Wabunge kutaka kulipwa mafao hayo ijumaa kabla ya bunge kumalizika.
    “Sijapata taarifa za Wabunge kutaka kulipwa gedha zao Ijumaa, ila natambua kuwa watalipwa baada ya kuvunjwa kwa Bunge hilo, kwani ndio utumishi wao utakuwa umefikia kikomo” Kippa.

    MWANANCHI
    Serikali imepandisha bei ya mafuta kuanzia leo baada ya jiji la Dar es Salaam kukumbwa na uhaba wa muda wa nishati hiyo kutokana na baadhi ya wafanyabiashara kusitisha mauzo kusubiri kunufaika na bei mpya.
    Mamlaka ya Udhibiti wa Hudama za Nishati na Maji (EWURA) ilitangaza jana kuwa kuanzia leo bei ya petroli imepanda kwa Sh232 kutoka bei ya sasa ya Sh1,966. Bei ya kikomo ya petroli sasa itakuwa Sh2,198, ikiwa ni ongezeko la asilimia 11.82.
    Bei ya dizeli imepanda kwa Sh261, ikiwa ni ongezeko la asilimia 14.65 na hivyo bei mpya itakuwa Sh2,043 badala ya Sh1,782, wakati mafuta ya taa yamepanda kwa Sh369 sawa na asilimia 22.75.
    Tangu bei ya mafuta ghafi ishuke hadi chini ya Dola 50 za Marekani kwa pipa mapema mwaka huu na kusababisha bei ya petroli kushuka hadi Sh1,652 mwezi Machi, mwenendo wa bidhaa hiyo imekuwa ni kupanda.
    Hadi jana, mafuta ghafi duniani yalikuwa yanauzwa chini ya Dola 60 za Marekani kwa pipa katika soko la dunia, lakini nishati hiyo nchini imerejea kwenye bei ambayo mafuta ghafi yalikuwa yakiuzwa Dola 100 kwa pipa.
    Mkurugenzi mkuu wa Ewura, Felix Ngamlagosi alisema mabadiliko aliyotangaza yanatokana na bei ya mafuta katika soko la dunia, pia kuendelea kudhoofika kwa thamani ya shilingi dhidi ya Dola ya Marekani pamoja na mabadiliko ya tozo za Serikali katika mafuta kuanzia Julai Mosi, 2015.
    Alisema thamani ya shilingi kwa machapisho ya bei za Juni na Julai 2015, imepungua kwa Sh 175.11 dhidi ya dola ya Marekani sawa na anguko la asilimia 8.65.
    “Juni mwaka huu bei za jumla petroli ziliongezeka kwa Sh232.35 kwa lita sawa na asilimia 12.49, dizeli Sh261.15 kwa lita sawa na asilimia 15.57 na mafuta ya taa Sh369.41 kwa lita sawa na asilimia 24.32,”Ngamlagosi.
    Pamoja na naibu waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage kutoa tamko kali bungeni kuonya wafanyabiashara dhidi ya vitendo vya kutouza mafuta, baadhi ya vituo vilikuwa havitoi huduma jana na juzi.
    Ewura ilisema jana inamfuatilia mtu aliyesambaza ujumbe kwa njia ya mitandao ya kijamii kutaarifu kuwapo kwa njama za wafanyabiashara kutouza mafuta kwa siku mbili kusubiri bei mpya.
    Ngamlagosi alisema Ewura imeiandikia barua Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Jeshi la Polisi kutaka wachunguze kujua ujumbe huo ili muhusika achukuliwe hatua.
    “Upungufu wa mafuta uliojitokeza mkoani Musoma na kuwasababishia usumbufu wananchi tunafuatilia na tukibaini watapewa adhabu ya kulipa faini ya Sh20 milioni au kwenda jela au kufutiwa leseni ya biashara ya mafuta,” Ngamlagosi.

    MWANANCHI
    Wanafunzi 18,751 waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka 2014, wamekosa nafasi ya kujiunga na shule za kidato cha tano kwa sababu mbalimbali ikiwamo ufinyu wa nafasi.
    Kati ya hao, wanafunzi 479 wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya ufundi huku idadi ya wanafunzi wa kike waliochaguliwa kujiunga na vyuo hivyo ikiongezeka kwa asilimia 25 kutoka wanafunzi 117 mwaka 2014 mpaka kufikia wanafunzi 147 mwaka huu.
    “Baadhi ya wanafunzi wamekosa nafasi kutokana na umri mkubwa na baadhi ya watahiniwa wa kujitegemea wanakosa sifa za kuchaguliwa,” Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Kassim Majaliwa alisema hapa jana alipokuwa akitangaza kuchaguliwa kwa wanafunzi hao.
    Alisema wanafunzi 55,003 sawa na asilimia 74.5 ya wanafunzi 73,754 waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka jana ndiyo waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano.
    Majaliwa alisema kuna ongezeko la ufaulu la wanafunzi 918 mwaka huu, ikilinganishwa na wanafunzi 54,085 waliochaguliwa mwaka 2014 kujiunga na kidato cha tano.
    Alisema wanafunzi waliokosa nafasi kuingia kidato cha tano watadahiliwa na Baraza la Taifa la Ufundi (Nacte) kwenye fani mbalimbali kama vile ualimu, afya, maendeleo ya jamii na kilimo.
    Alisema ufaulu wa watahiniwa wa kidato cha nne mwaka 2014 kuanzia daraja la ‘distinction’ hadi ‘credit’, yaani ufaulu wa wastani (GPA) wa 5.0 hadi 1.6 ni watahiniwa 73,754 sawa na asilimia 37.4 ya wanafunzi 240,410 waliofanya mtihani huo.
    Alisema uchaguzi ulifanyika kwa kufuata machaguo matano ya tahasusi (combinations) yaliyojazwa na wanafunzi kwenye fomu ya uchaguzi ‘Selform.’
    Alisema mfumo wa kompyuta ulitumika katika kumpanga mwanafunzi katika uchaguzi wake wa masomo na shule kwa kuanzia na chaguo la kwanza. “Kama mwanafunzi atakuwa hana sifa katika machaguo yote aliyoomba, hupangiwa chaguo la somo alilofaulu zaidi na katika shule iliyopo karibu na wilaya yake ya makazi kulingana na tahasusi na nafasi zilizopo,” alisema Majaliwa.
    Alisema wanafunzi 29,744 watajiunga na masomo ya sayansi na 25,259 watajiunga na masomo ya sanaa na biashara.
    Aliwataka wanafunzi waliochaguliwa kuripoti katika shule walizopangiwa ili kuanza muhula wa kwanza wa masomo unaotarajiwa kuanza Julai 18.
    “Naagiza wanafunzi wote kuripoti katika shule walizopangiwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti kwa zaidi ya wiki mbili kuanzia tarehe ya mwisho ya kuripoti, nafasi yake itachukuliwa na mwanafunzi mwingine aliyekosa nafasi,” alisema Majaliwa ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa, Lindi.

    MWANANCHI
    Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ameamua kutoa ufafanuzi wa sakata la mabilioni kutoka Libya ambayo amekuwa akihusishwa nayo, akieleza kuwa fedha zote zilizotolewa kwa amri ya mahakama ni mkopo na hazikuchotwa kama ilivyokuwa kwenye kashfa za Epa au Escrow.
    Membe amekuwa akihusishwa na fedha hizo, Dola 20 milioni za Marekani (sawa na Sh40 bilioni) ambazo zilikuwa zimehifadhiwa katika akaunti ya Libya No.004-200-0002216-01 iliyokuwa Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB).
    Kwa mujibu wa waraka alioutoa jana kwa vyombo vya habari kuhusu fedha hizo, Membe alisema Serikali ya Libya na Tanzania zilitia sahihi mkataba wa nyongeza (Addendum to the Dept Swap Agreement) ambao ulizungumzia, pamoja na mambo mengine, matumizi ya fedha hizo.
    Mkataba huo wa nyongeza unatamka katika kifungu No.4.02, kwamba, fedha hizo zikopeshwe kwa mwekezaji aliyeteuliwa na Libya, ambaye ni kampuni ya Meis Industries Limited kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa kiwanda cha Saruji mkoani Lindi.
    “Ni mkopo uliotolewa kwa Kampuni ya Meis kwa mujibu wa Mkataba wa Makubaliano (Investment Agreement) wenye masharti ya kibenki. Na Masharti hayo ya kibenki yanamtaka mwekezaji kuweka dhamana, kulipia riba, kuwekewa muda wa kurudisha mkopo, na anawekewa hatua za kuchukuliwa endapo mwekezaji huyo atashindwa kulipa mkopo,” Membe.
    “Kwa lugha nyingine, kampuni ya Meis ikishindwa kulipa mkopo huo, itafilisiwa mali zake na TIB itarudishiwa fedha zake. Iacheni benki ifanye kazi yake. Mkopo unageukaje kuwa ufisadi?”
    Membe alisema yeye hana kampuni hapa nchini, hana ubia na kampuni yoyote, pia hana hisa katika kampuni ya Meis na hajafaidika na mkopo huo ambao unasimamiwa na TIB.
    “Ndiyo maana uvumi kuwa nahusika na ufisadi wa mabilioni ya Libya hauna mashiko kabisa. Baadhi ya wanasiasa wenzangu wanajua ukweli wote huu, lakini kwa makusudi wanaamua kuwafanya watu waamini,” Membe.
    Anasema ujenzi wa kiwanda cha saruji cha Lindi unaendelea vizuri na mitambo yote inayotakiwa katika ujenzi huo imeshawasili.
    “Asilimia 45 ya ujenzi wa kiwanda hicho umekamilika na ni mategemeo ya kampuni ya Meis kuwa kiwanda hicho kitakamilika ifikapo Desemba mwaka huu wa 2015,” anasema.
    Alisema kumbukumbu zinaonyesha mambo mawili, kwamba, kabla ya Serikali ya Libya kutia sahihi nyongeza hiyo ya mkataba iliyotaka fedha zikopeshwe kwa Meis, upembuzi yakinifu wa mradi husika ulifanywa na Libya kupitia vyombo vyake, walishajiridhisha juu ya ubora wa mradi huo.
    Pili alisema baada ya kutia sahihi nyongeza ya mkataba, serikali ya Libya kupitia ubalozi wake hapa nchini iliendelea kusisitiza kwa maandishi kwamba Serikali ya Tanzania iharakishe mchakato wa kuwezesha fedha hizo zikopeshwe kwa mwekezaji waliyemteua ili mradi huo muhimu usiendelee kuchelewa, na pia fedha ziingie katika mzunguko kwa manufaa ya Watanzania.

    NIPASHE
    Mbunge wa Songea Mjini, Emmanuel Nchimbi, ametamka rasmi kuwa azma ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
    Taarifa ya Nchimbi iliyopatikana kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii jana ilieleza kuwa, baada ya kuwa katika shinikizo kubwa kutoka kwa viongozi na wananchi waliomuamini ili agombee nafasi hiyo, amemua kutogombea.
    “Mpaka  jana waliochukua fomu wamefikia 41, nimewaangalia wote waliochukua fomu na nimeridhika kuwa hatutaweza kumkosa Rais bora miongoni mwao, hivyo nimeamua kutogombea,” alisema.
    Aliongeza, “Nimefanya uamuzi huu nikiamini kwamba bado ninayo fursa ya kuwatumikia Watanzania na kuleta maendeleo kwa namna nyingine.”
    Nchimbi ambaye ni miongoni mwa watu waliokuwa wakitajwatajwa kutaka kuwania urais kupitia CCM katika taarifa yake hiyo aliwaomba radhi waliomshawishi, waliomwamini na kutarajia kuwa angegombea nafasi hiyo ya juu katika utawala wa nchi.
    Nchimbi anatajwa kama mwanasiasa kijana mzoefu wa CCM akiwa amekuwa mjumbe wa Kamati Kuu kwa zaidi ya miaka 10 pia akiwa Mwenyekiti wa Vijana wa CCM kwa vipindi viwili na sasa mjumbe wa  Nec.
    Kwa kauli ya Nchimbi ni kama ametangazia dunia kwamba kuna timu anaiunga mkono ingawa hajawa tayari kuitangaza.
    Wakati huo huo, Nchimbi anakibarua kigumu cha kuamua jimbo atakalogombea mwaka huu kati ya jimbo lake la sasa la Songea Mjini na lililokuwa likishikiliwa na Maraehemu John Komba aliyefariki dunia Aprili, mwaka huu la Mbinga Magharibi.
    Nchimbi aliwaacha njiapanda wapiga kura wa jimbo hilo baada ya kusema hajajua atagombea jimbo gani kati ya hayo mawili.

    NIPASHE
    Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), anayeomba kuteuliwa na chama hicho kugombea urais, January Makamba, amesema mgombea  urais ‘anayemwaga’  fedha na kufanya ‘mbwembwe’ ili kushawishi wananchi wamchague, hafai kuiongoza Tanzania.
    Aidha, Makamba amesema ikiwa atafanikiwa katika nafasi anayoiomba, atahakikisha anasimamia ujenzi wa reli kutoka Mtwara hadi Ruvuma pamoja na kufufua bandari.
    Amesema ujenzi wa reli ni muhimu kwa kuwa utasaidia kurahisisha usafirishaji wa mazao na mizigo mingine katika mikoa mbalimbali ya Tanzania.
    Alisema Bandari ya Mtwara imesahaulika kwa kipindi kirefu na inarudisha nyuma maendeleo ya mikoa ya Kusini ambayo  ilisahaulika miaka ya nyuma.
    Makamba aliyasema hayo jana mjini hapa alipokuwa akisaka wadhamini ili kumwezesha kupata sifa ya kufikiriwa kuteuliwa na CCM kugombea urais.
    “Mtu anayemwaga fedha na kuonyesha mbwembwe nyingi, hafai kuiongoza nchi kwa kuwa akiingia Ikulu hatalisaidia taifa,”.
    Alisema zao la korosho ni lazima liwafaidishe wananchi wa Mtwara kwa kuwa katika kipindi kirefu wakulima wamekuwa wakipunjwa kwa kupewa bei ndogo.
    Umati mkubwa uliokuwa ukimsikiliza Makamba, ulilipuka kwa shangwe baada ya kusikia kauli za matumaini hususani namna atakavyosaidia wananchi kunufaika na zao la korosho na ujenzi wa miundombinu.
    Kuhusu zao la korosho, Makamba aliahidi kufufua viwanda vya kubangulia zao hilo ili kulipa thamani na kuachana na utaratibu wa sasa.
    Kwa sasa zao la korosho linabanguliwa nje ya nchi, hatua ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wakulima kwamba inawakandamiza kwa miaka mingi na kuwafanya kuiuza kwa bei ya kutupa.

    HABARILEO
    Kijana mpya wa Arsenal, Petr Cech amepokea vitisho kibao vya kutaka kuuawa kutoka kwa mashabiki wa Chelsea kufuatia kukamilika kwa mpango wa kutua Emirates kwa dau la pauni milioni 10.
    Mashabiki walituma vitisho hivyo katika mtandao ya kijamii kupitia ukurasa wake waTwitter wakionyeshwa kukerwa na kitendo cha kipa huyo kuhamia kwa mahasimu wao wa jiji la London, Arsenal.
    Mashabiki wa Chelsea wameonekana kutofurahishwa na uamuzi huo wa Cech kuhamia katika klabu nyingine ya London licha ya mchezaji huyo wa kimataifa kuichezea klabu hiyo kw amafanikio makubwa wakati wa kipindi chake cha miaka 11 hapo Stamford Bridge.
    Watumiaji wa Twitter walimbatiza Cech jina la msaliti na kumuita nyoka wakati wengine wakisema Cech amekufa huku sura yake wakiwa wameivalisha kinyago cha sura ya nyoka.

    Tuesday, 30 June 2015

    Maneno ya utani ya Rais Mugabe kwa Obama baada ya kuruhusu ndoa ya jinsia moja

    mugabe
    Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe
    Ndani ya wiki moja baada ya Serikali ya Marekani kupitisha sheria ya kuruhusu ndoa ya jinsia moja kwa raia wake kumekuwepo na maoni mbalimbali kutoka kwa watu kuhusiana na maamuzi hayo.
    Mmoja wa watu walioguswa na maamuzi hayo ni Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe ambaye ameeleza hisia zake baada ya maamuzi hayo kupitishwa.
    obama
    Rais wa Marekani Barack Obama
    Katika mahojiano na radio ya Taifa ya Zimbwabwe, Mugabe alisema hawezi kupingana na maamuzi ya nchini hiyo kwani ni sheria ambayo imepitishwa na Serikali na kama ni hivyo ataamua kufunga safari kwenda jijini Washington kuomba kufunga harusi na Rais Barack Obama.
    Ameongeza kuwa, Serikali ya Marekani imekuwa ikiongozwa na wajinga ambao ni  wafuasi wa shetani wanayoitukana taifa la Marekani akisisitiza Marekani imechafuka na wanaiendesha nchi kwa dhana zao binafsi ambazo ni dhana potofu.

    Hizi ndio sababu za Facebook kuamua kufungua office zao South Africa

    Facebook-Headquarters
    Nimeipata hii takwimu ambayo sikuwa nafahamu, kumbe Facebook ina watumiaji Milioni 120 wa Mtandao huo ndani ya Africa pekeyake !!
    Story nyingine kuhusu Facebook kwa sasa hivi ni ishu ya kusogeza Office zao mpaka ndani ya Jiji la Johannesburg Afrika Kusini na tayari hapo ndio yatakuwa Makao Makuu ya shughuli zao zote zinazohusu Facebook Afrika, Nunu Ntshingila ndio Boss ambaye kachukua ajira kusimamia Kampuni hiyo.
    enter-facebook-office
    Mark Zuckerberg, Boss wa Facebook
    Kingine ni kwamba jamaa wameamua kuisogeza Facebook ndani ya Afrika kama njia ya kusogea karibu ya wateja wao wengi ambao ni Wafanyabiashara wanaotumia Mtandao huo katika kutangaza biashara zao.
    Facebook-opens-first-African-o
    Facebook iliangalia siku nyingi sana jinsi ya kuingia kwenye soko la Afrika, waliwahi kurahisisha huduma kwa watumiaji wa mtandao huo kwa kuweka App maalum ambayo mtumiaji hakatwi pesa wala hatumii data kwenye kuchat, mpango wao mwingine ni kuhakikisha wanamfikia kila mtu hata ambae hana uwezo wa kumiliki simu yenye uwezo wa Internet.

    TAHADHARI KWA UMMA KUHUSU MATAPELI KWA NAFASI ZA KAZI TANESCO


    Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linapenda kutoa tahadhari kwa Umma kuwa kuna mtu/watu wanatumia jina la TANESCO vibaya kwa kutumia namba mbalimbali za Simu na barua pepe kuwadanganya wananchi kuwa TANESCO imetangaza nafasi za kazi na wanaweza kuwasaidia kupata kazi hizo.
    Barua pepe inayotumiwa na watu/mtu huyo inasomeka francisnelson884@yahoo.com na Jeremiapeter896@yahoo.com. Watu/mtu huyo hudai fedha ili aweze kutoa msaada wa kumwezesha mtu apate kazi TANESCO.
    Shirika linawatahadharisha wananchi wote kwa ujumla kuwa halina utaratibu wa kutangaza nafasi za kazi kwa kuwatumia watu barua pepe au kuwapigia simu au hata kudai kiasi chochote cha fedha ili kumpatia mtu ajira. TANESCO inafuata taratibu zote za Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini katika mchakato wote wa kuajiri. Taratibu za Shirika ni kutangaza nafasi za kazi kupitia magazeti ya kila siku pamoja na kuweka tangazo husika katika Tovuti, Blog, Twitter na Facebook akaunti za Shirika ambazo ni www.tanesco.co.tz ;www.umemeforum.blogspot.com; www.twitter.com/tanescoyetu ; www.facebook.com/tanescoyetu
    Wakati uchunguzi kwa matapeli hao unaendelea, TANESCO inasisitiza kuwa haina Uhusiano wowote na watu/mtu huyo ambaye kisheria ni tapeli na mwenye lengo la kuharibu sifa nzuri ya Shirika.
    Uongozi unaendelea kuwatahadharisha wale wote wanaoomba nafasi za kazi ndani ya Shirika kuwa makini na matapeli hao na kufuata utaratibu uliowazi uliowekwa na Shirika.
    Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano
    TANESCO Makao Makuu.