Shirika
la Umeme Tanzania (TANESCO) linapenda kutoa tahadhari kwa Umma kuwa
kuna mtu/watu wanatumia jina la TANESCO vibaya kwa kutumia namba
mbalimbali za Simu na barua pepe kuwadanganya wananchi kuwa TANESCO
imetangaza nafasi za kazi na wanaweza kuwasaidia kupata kazi hizo.
Barua pepe inayotumiwa na watu/mtu huyo inasomeka
francisnelson884@yahoo.com na
Jeremiapeter896@yahoo.com. Watu/mtu huyo hudai fedha ili aweze kutoa msaada wa kumwezesha mtu apate kazi TANESCO.
Shirika
linawatahadharisha wananchi wote kwa ujumla kuwa halina utaratibu wa
kutangaza nafasi za kazi kwa kuwatumia watu barua pepe au kuwapigia simu
au hata kudai kiasi chochote cha fedha ili kumpatia mtu ajira. TANESCO
inafuata taratibu zote za Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini katika
mchakato wote wa kuajiri. Taratibu za Shirika ni kutangaza nafasi za
kazi kupitia magazeti ya kila siku pamoja na kuweka tangazo husika
katika Tovuti, Blog, Twitter na Facebook akaunti za Shirika ambazo ni www.tanesco.co.tz ;www.umemeforum.blogspot.com; www.twitter.com/tanescoyetu ; www.facebook.com/tanescoyetu
Wakati
uchunguzi kwa matapeli hao unaendelea, TANESCO inasisitiza kuwa haina
Uhusiano wowote na watu/mtu huyo ambaye kisheria ni tapeli na mwenye
lengo la kuharibu sifa nzuri ya Shirika.
Uongozi
unaendelea kuwatahadharisha wale wote wanaoomba nafasi za kazi ndani ya
Shirika kuwa makini na matapeli hao na kufuata utaratibu uliowazi
uliowekwa na Shirika.
Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu.
0 comments:
Post a Comment