Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu dompromo@gmail.com au Whatsapp namba +255759399445.
Hatimaye
baraza kuu la Chadema limeridhia kusimama kwa muda kufanya kazi za
chama aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho Dr Wilbrod Slaa.
Ni
kishindo cha baraka za baraza kuu la Chadema likiridhia kupumzika kwa
Dk Wilibroad Slaa ambaye tangu kujiunga kwa wazir mkuu mstaafu Edward
Lowassa amekuwa haonekani katika vikao vyetu vya chama hicho, katika
ufunguzi wa mkutano wa baraza kuu la Chadema mwenyekiti wa chama hicho
taifa Freeman Mbowe amekiri kuwa licha ya Dkt Slaa kushiriki vikao
mbalimbali vya chama kuhusu ujio wa lowassa, lakini ni kweli
alitofautian kimtizamo na wajumbe wa kamati kuu.
Aidha
Freeman Mbowe amekiri pia juu ya hofu iliyokwisha kutanda kwa viongozi,
wanachama na wapenzi wa chama hicho juu ya ujio wa baadhi ya vigogo
kutoka ndani ya chama cha mapinduzi CCM.
Kwa
upande wake kaimu katibu mkuu wa Chadema taifa Salum Mwalimu
akizungumza katika mkutano huo pamoja na masuala mengine amewataka
wanachama na wapenzi wa chama hicho kuahkikisha wanaunganisha nguvu hasa
katika kipindi cha uchaguzi.
Miongoni
mwa agenda kuu zilizojadiliwa katika baraza kuu la Chadema ni pamoja na
agenda ya kupitisha ilani ya chama hicho, kupendekeza majina ya
wagombea nafasi ya urais ikiwa ni pamoja na kuthibitisha mikakati na
rasilimali za kuendesha kampeni za uchaguzi mkuu.
0 comments:
Post a Comment