
Flash ya Corsair
Kama umeweka vitu
vyako vingi vingine vya siri zako kabisa kwenye kitu kama memory card,
flashdisk na external hard disk, ikatokea bahati mbaya kifaa hicho
kikapotea ni lazima utachanganyikiwa kutokana na kupoteza kitu chako
chenye vitu muhimu!
Kampuni ya Toshiba na Corsair
wametoa flash disks zenye keypad, halafu kingine ni kwamba hii
itakuwezesha kuweka password katika flash yako, hakuna mtu mwingine
ataweza kuifungua na kuona kilichomo ndani zaidi ya wewe mwenyewe
unaezijua namba za siri.
Iwapo mtu akijaribu
kuingiza password zaidi ya mara kumi flash hiyo itafuta data zote
zilizomo, hii itakusaidia kama kuna vitu vya siri basi hakuna
atakayeweza kuvitoa.

Flash ya Toshiba
Toshiba
imesema itaingiza sokoni flash hizo ambazo zitakuwa na ukubwa wa
kuanzia 4GB, 8GB, 16GB na 32GB, upande wa bei pia ni kuanzia dola95
(laki 170,ooo/= Tshs) hadi dola 200 (360,000= Tshs)
0 comments:
Post a Comment