
Kutoka Nollywood, story hazikuwa kwa
siku ya leo, wengi huenda hawakuamini kutokana na uvumi uliokuwa ukienea
mitandaoni kwamba muigizaji Muna Obiekwe
amefariki, lakini huo ulikuwa uvumi ambao ulikanushwa, hii ilitokana na
muigizaji huyo kuumwa kwa muda mrefu ambapo alikuwa akisumbuliwa na
tatizo la figo.
Staa huyo wa filamu za Nigeria amefariki jana mchana akiwa hospitali jijini Lagos kutokana na ugonjwa huo wa figo.
Ugonjwa wake ulifahamika na wasanii
wenzake pamoja na ndugu zake, kuna wakati aliwahi aliwaambia marafiki
zake kwamba amepanga kuandaa show ya maigizo ya jukwaani ili kupata
fedha za matibabu.
0 comments:
Post a Comment